Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

WAZIRI APIGWA KOFI UFARANSA

06:30 Add Comment

Waziri mkuu mstaafu wa Ufaransa Manuel Valls amekashifiwa alipokuwa akihamasisha katika kampeni za chama cha kisoshalisti katika uchaguzi mkuu wa kiti cha Urais nchini Ufaransa.
Alipokuwa akihutubia katika ukanda wa Magharibi mwa mji wa Brittany alipigwa kofi na kijana mdogo alipokuwa akisalimia kwa kushikana mikono.
Mlinzi binafsi wa Bwana Valls alimkamata kijana huyo kooni kisha akamtupa chini.
Manuel Valls hajajeruhiwa katika tukio hili.

WAFUNGWA 30 WAFARIKI KATIKA MACHAFUKO BRAZIL

06:14 Add Comment

Taarifa za kutisha zimeanza kujitokeza nchini Brazil kutokana na machafuko yaliyotokea usiku kucha katika jela la Alcaçuz baada ya kuibuka kwa mgomo.
Mamlaka nchini Brazil zinasema takriban wafungwa thelathini waliuawa na wafungwa wenzao, wataalamu wakuchunguza masuala ya mauwaji wamesema walioathirika zaidi walikuwa wamekatwakatwa au kutolewa baadhi ya viongo.
Mgomo huo ulianza jumamosi mchana, wanakikundi wa kikundi cha wahalifu waliopo katika magereza ya Brazil na kushambulia kundi hasimu lenye msimamo tofauti.
Hii ni mara ya tatu kwa mgomo mkubwa kama huu kujitokeza kwa wafungwa nchini Brazil mwezi huu, mamia ya wafungwa wamefariki gerezani katika miji ya Amazonas na Roraima.

UTAMBUE MJI WA KWANZA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA

16:46 Add Comment

Mji wa Auckland nchini New Zealnd ndio mji wa kwanza duniani kuukaribisha mwaka mpya wa 2017.
Fataki zilirushwa kutoka jengo refu katikati mwa mji huo.
Polynesia na visiwa vya Pacific ikiwemo Samoa, Tonga na kiribati pia viliukaribisha mwaka mpya.
Miji mingi duniani imeimarisha usalama kwa sherehe za mkesha wa mwaka mpya baada ya mwaka ambapo washambuliaji waliendesha malori katika umati wa watu mjini Berlin na Nice.
Mjini Paris Madrid na New York vizuizi vya simiti na magari yaliobeba mizigo mizito yatatumiwa kuzuiwa bustani zilizopo mjini ambapo watu wengi hukongamana ili kusherehekea.

KIJANA ALIEPANGA KUMUUA TRUMP AFUNGWA

06:18 Add Comment

Mwanamme mmoja raia wa Uingereza amehukumiwa kifungo cha miezi 12 jela kufuatia jaribio lake la kutaka kunyakua bunduki kwa lengo la kumuua Donald Trump.
Michael Sandfgord mwenye umri wa miaka 20 alikiri makosa hayo ya kumiliki bunduki na kuvurua mkutano.
Analaumiwa kwa kujaribu kunyakua bunduki kutoka kwa polisis wakati wa mkutano wa hadhara huko Las Vegas ili kumfyatulia risasi mgombea urais.

Mahakama ilisema kuwa huenda akaachiliwa baada ya miezi minne ambapo atasafirishwa hadi nchini Uingereza
Baada ya Sandford kukamatwa aliwaambia maafisa kuwa alikuwa na mpango wa kumpiga risasi Donald Trump.
Hata hivyo hakufanikiwa kunyakua bunduki kutoka kwa afisa wa polisi.
Mamake alisema kuwa alikuwa amepoteza mawasiliano na mwanawe, ambaye aliondoka nyumbani kutembea kote marekani mwaka 2015.
Kulingana na nyaraka za mahakama Sandfords ambaye hakuwa na makao na ambaye alikuwa akiishi Marakani kinyume na sheria baada ya muda wa visa yake kuisha, aliiwaambia majasusi kuwa aliendesha gari kutoka California hadi Nevada kwa lengo la kumpiga risasi Trump.
Anaripotiwa kumuambi afisa wa polisi kuwa alitarajia kuuawa kwenye shambulizi hilo na kwamba alikuwa na tikiti za kuhudhuria mkutano mwingine wa Trump baadaye ikiwa angapata fursa ya pili.
Majaji walitaja kitendo hicho kuwa cha kustaajabisha.

AGUERO OUT MECHI NNE

23:34 Add Comment

Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero amepigwa marufuku kucheza mechi nne baada yake kufukuzwa uwanjani kwa uchezaji mbaya mara ya pili msimu huu.
Aguero, 28, alifukuzwa uwanjani kwa kumchezea visivyo beki wa Chelsea David Luiz wakati wa mechi ambayo City walilazwa 3-1 nyumbani Ligi ya Premia siku ya Jumamosi.
Mshambuliaji huyo wa Argentina alikuwa ameadhibiwa tena mwezi Agosti alipopewa kadi nyekundu kwa kumchezea visivyo mchezaji wa West Ham Winston Reid.
Atakosa mechi za City dhidi ya Leicester, Watford, Arsenal na Hull.

Mwenzake wa City Fernandinho pia alifukuzwa uwanjani alipokabiliana na Cesc Fabregas baada ya madhambi hayo ya Aguero na amepigwa marufuku kucheza mechi tatu.

MITANDAO KUDHIBITIWA

23:31 Add Comment

Kampuni kubwa za kiteknolojia Duniani zimeanzisha programu mpya itakayosaidia kupunguza kasi ya uchochezi na misimamo mikali mitandaoni.
Twitter, Facebook, na Microsoft watakapo baini kuwepo kwa taarifa za aina hiyo wata zitambulisha kwa alama maalumu.
Suala hili litahimiza umakini ili kurahisisha utambuzi wa taarifa chochezi zitatokea katika mitandao yao.
Kampuni hizo zimearifu kuwa mchakato huo hauta jiendesha wenyewe ili kuepusha upotoshaji usiotarajiwa kwa waandishi na taarifa nyingine zinazo ashiria vurugu japo kuwa hazi chochei moja kwa moja

MZOZO WA MPAKA KATI YA MALAWI NA TANZANIA WAIBUKA TENA

21:15 Add Comment

Ramani mpya iliyotolewa na Tanzania ambayo inaonyesha kuwa inaamiliki nusu ya Ziwa linalozozaniwa la Malawi au Nyasa, imezua mzozo mpya na Malawi ambayo inasema kuwa ramani hiyo sahihi.
Ramani ya Tanzania inaonyesha kuwa eneo la Kaskazini Mashariki mwa ziwa hilo ni sehemu ya himaya yake, lakini Malawi nayo inadai kuwa eneo hilo lote ni lake.
Malawi imeomba Umoja wa Mataifa, Mungano wa Afrika na mashirika mengine ya kimataifa kuingilia kati.
Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Malawi, Rejoice Shumba amesema kuwa Malawi imeandika barua kwa mashirika makuu duniani ikiyataka kupuuzilia mbali ramani ya Tanzania.
Hii si mara ya kwanza Malawi imepinga ramani hiyo ya Tanzania.
Msukosuko uliibuka mwaka 2011 wakati Malawi ilianza shughuli za kutafuta mafuta kwenye ziwa hilo.
Serikali ya Tanzania bado haijatamka lolote kukuhusu suala hilo.
Nini hasa kinazozaniwa?
Fahari ya nchi na maswala ya kujiendeleza kiuchumi kwa Malawi na Tanzania kila mmoja akisimama kidete kusisitiza msimamo wake.
Kwa Tanzania, ziwa hilo linajulikana kama Nyasa, wakati nchini Msumbiji inajulikana kama Lago Niassa.
Malawi na Tanzania ni koloni za zamani za Uingereza wakati Msumbiji ilikuwa chini ya ukoloni wa Ureno. Uingereza iliichukua Tanzania kutoka kwa Wajerumani baada ya wao kushindwa katika vita vya kwanza vya dunia.
Kando na ripoti za kuwepo mafuta na gesi katika ziwa hilo, ziwa lenyewe ni kivutio kikubwa cha watalii.
Malawi inasema inashauriana na Msumbiji kuhusiana na uchimbaji wa mafuta katika siku za baadaye ili kuzuia mzozo wa kidiplomasia .
Je hii ni mara ya kwanza kwa mzozo huu wa ziwa Malawi kutokea?
Hapana. Mapema miaka ya sitini, Malawi ilidai umiliki wa ziwa hilo kwa kuambatana na makubaliano ya mwaka 1890 Heligoland kati ya Uingereza na Ujerumani ambayo yalisema kuwa mpaka kati ya nchi hizo uko upande wa Tanzania.
Makubaliano hayo yaliafikiwa na Muungano wa Afrika na Tanzania ikaitikia ingawa shingo upande. Mzozo mpya kati ya nchi hizo ukaripotiwa tena kati ya mwaka 1967 na 1968.
Ulichipuka tena mwaka mwaka 2011, Malawi ilipotoa leseni ya kuchimba mafuta kwa kampuni ya British Surestream Petroleum Limited. Sehemu iliyotolewa kwa uchimbaji wa mafuta ni sehemu yenye mraba wa kilomita 20,000 sehemu ambayo Tanzania inasema ni yake.
Vyombo va habari viliripoti mwezi Julai mwaka 2012 kuwa mitumbwi ya wavuvi na ya watalii kutoka Malawi ilivuka na kuingia upande wa Tanzania
Tanzania nayo ikasema kuwa ingetafuta ushauri kutoka jamii ya kimataifa ikiwa nchi hizo hazingeweza kusuluhisha mzozo huo zenyewe.
Hofu ya hatua za kijeshi
Hofu ya mzozo kutokota na kuwa mbaya zaidi ilijitokeza mwaka 2012 wakati Tanzania iliposema kuwa ingelinda mipaka yake na kuzingatia sheria za kimataifa.

KIONGOZI WA UPINZANI ASHINDA UCHAGUZI WA URAIS GAMBIA

05:44 Add Comment

Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Gambia amemtangaza mgombea wa upinzani Adama Barrow, kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa mwaka 2016.
Adama Barrow alipata kura 263,515 huku Rais Yahya Jammeh akipata kura 212,099
Mwandishi mmoja wa habari kutoka shirika la Reuters anasema kuwa amezungumza na Adama Barrow aabaye amemuambia kuwa anasubiri simu ya kukubali kushindwa kutoka kwa bwana Jammeh.
Waziri wa masuala ya ndani nchini Gambia na mkuu wa polisi wamehutubia taifa wakitaka kuwepo utulivu.
Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Gambia amewaambia waandishi wa habari kuwa Rais Yahya Jammeh ambaye ameitawala nchi kwa miaka 22 baada ya kuingia madarakani kwa njia ya mapinduzi atakubali kushindwa.

FIDEL CASTRO AMEAGA DUNIA

10:14 Add Comment

Kiongozi wa Cuba Mwanamapinduzi Fidel Castro amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika jijini la Havana. Kifo hicho kimethibitishwa kwenye taarifa iliyotolewa televisheni ya taifa nchini humo na ndugu yake Rais Raul Castro.
Kiongozi Mkuu huyo wa Mapinduzi ya Cuba amefariki dunia majira ya saa nne usiku kuamkia le akiwa na umri miaka 90.

KANYE WEST ALAZWA HOSPITALI LOS ANGELES

06:06 Add Comment

Mwanamuziki mashuhuri nchini Marekani Kanye West amelazwa hospitalini mjini Los Angeles, vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti.
Msemaji wa polisi ameambia BBC kwamba walipokea simu ya kutokea kwa mtafaruku Jumatatu adhuhuri, lakini hawakutaja jina la mwanamuziki huyo.
Baadaye, mtafaruku huo ulidaiwa kuwa tukio la kimatibabu, na maafisa wa kutoa huduma ya dharura walifika eneo hilo.
Msemaji wa maafisa wa huduma za dharura wa LA amesema mwanamume ambaye jina lake halikutajwa alipelekwa hospitalini "kufanyiwa uchunguzi zaidi".
"Mwendo wa saa 13:20 majira ya kanda ya pasifiki, idara ya huduma za dharura ya Los Angeles ilipokea ombi la dharura la huduma ya matibabu ambalo halikuelezwa kwa kina," amsemaji huyo alisema.
"Mwanamume mzima, ambaye hali yake ya afya ni thabiti, alipelekwa hospitalini kufanyiwa uchunguzi zaidi."
NBC news wanasema hatua ya kumlaza West imechukuliwa kwa ajili ya afya yake na usalama wake.
Tovuti ya udaku ya TMZ imesema West amepelekwa hospitali kufanyiwa "uchunguzi wa kiakili" na kwamba amekuwa akitafuta matibabu "kwa sababu ya kukosa usingizi sana".
Los Angeles Times imeripoti kwamba kulipigwa simu ya 911 kutoka nyumba ya Kanye West.
West nawawakilishi wake hawajazungumzia tukio hilo.
Mkewe, Kim Kardashian, alitarajiwa kuhudhuria hafla fulani New York Jumatatu, mara yake ya kwanza kutokea hadharani tangu avamiwe na wezi Paris mwezi Oktoba, lakini hakufika.
West alikuwa amefuta tamasha zote zilizokuwa zimesalia kwenye ziara yake ya sasa ya kimuziki.
Alikuwa ameondoka tamasha ya Sacramento ikiwa katikati wikendi.
Alikuwa ameimba nyimbo tatu pekee Jumamosi usiku kabla ya kuanza kuwafokea watu na kushambulia Facebook, Jay Z na Hillary Clinton.
Alimkosoa mkuu wa Facebook Mark Zuckerberg kwa kukosa kumlipa $53m (£42.5m) alipe madeni.
Alisema pia kwamba alikereka sana na hatua ya Jay Z na familia yake kutomtembelea baada ya mkewe kuporwa Paris mwezi Oktoba.

PAPA FRANSISCO ASOGEZA MBELE KUSAMEHEWA KWA WANAWAKE WALIOTOA MIMBA

06:25 Add Comment

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amesogeza mbele kwa muda usiojulikana suala la mapadre wa kikatoliki duniani kusamehe wanawake walitoa mimba.
Mwaka jana aliwaruhusu mapadre kufanya hivyo kwa kipindi ambacho kilitajwa kama mwaka wa huruma ya Mungu kilichoisha Jumapili iliyopita.
Hapo awali maaskofu peke yao ndio waliokuwa na uwezo wa kuwasamehe wanawake waliotoa mimba.
Baba mtakatafu amesisitiza kwamba mafundisho ya kikatoliki yanaonyesha kwamba utoaji mimba ni kosa kubwa, lakini kiongozi huyo ameeleza kwamba Mungu ni mwenye huruma na anaweza kusamehe dhambi zote ikiwa mkosaji atatubu.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani amesema anaelewa jinsi suala la utoaji wa mimba linavyoweza kuwa tatizo kimaadili kwa mwanamke.

MUGABE: WATU WANAOMBA NIFE

06:22 Add Comment

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, mwenye umri wa mika 92, anazungumzia kuhusu kustaafu , lakini swali ambalo bado watu wanahoji ni ikiwa kweli anamaanisha hilo.
Mwishoni mwa juma Bwana Mugabe aliuambia mkutano wa watu wapatao 400- walio piagania uhuru kwamba ikiwa atastaafu anapaswa kupewa fursa "inayofaa" kufanya hivyo.
Pia aliwakosoa baadhi ya viongozi wa chama chake cha Zanu-PF kwa kumuombea afe na kujaribu kumroga ili wachukue nafasi yake.
Malumbano ya ndani kwa ndani miongoni mwa wafuasi wa chama tawala ya kutaka kumrithi Bwana Mugabe yameongezeka huku kiongozi huyo akionekana kuendelea kudhoofika zaidi.
Lakini si mara ya kwanza Kwa Bwana Mugabe kuongelea kuhusu kuachia madaraka.

Mwaka 2006 alitangaza kuwa atagombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2008.
Licha ya hayo aligombea na kushinda katika uchaguzi uliokuwa na ghasia ambao matokeo yake yalibishaniwa.
Kwa hivyo haijawa wazi ni lini , kama kweli Rais Mugabe ataondoka madarakani.
Mnamo mwishoni mwa juma kamati za kikanda za chama tawala cha, Zanu-PF zilimuidhinisha kama mgombea wake katika uchaguzi wa 2018, ambapo atakuwa na umri wa miaka 94.
Chama hicho kitaidhinisha uamuzi huo katika mkutano mkuu wa chama utakaofanyika mwezi ujao.
Kwa hiyo kwa sasa haionekani kama kweli anaangalia uwezekano wa kustaafu.
Utawala wa rais Mugabe umekuwa ukikabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kushuka kwa sarafu ya nchi hiyo.
Hali mbaya ya uchumi na ukosefu wa ajira vilisababisha maandamano makubwa kote nchini humo, wanaharakati na raia kwa ujumla wakimtaka rais Mugabe aachie mamlaka.
Hata hivyo Mugabe amekuwa akiyazima maandamano hayo na kuwatia nguvuni wapinzani wake anaosema kuwa wanachochewa na mataifa ya kigeni. kutokana na vikwazo kutoka mataifa ya magharibi.
Mugabe amekuwa akikosolewa kwa kukandamiza upinzani.

MTOTO KUZALIWA BILA MAMA?

13:29 Add Comment

Wanasayansi wanasema kuwa majaribio ya awali yanaonyesha kuwa siku za usoni itawezekana kuwatengeneza watoto bila ya kutumia mayai ya mama.
Wanasayansi hao wamefaulu kutengeneza watoto wa panya kwa kutumia mbegu za kiume na kuziunganisha na seli za kawaida kwa kuzidanganya kudhani kwamba zitatungisha mayai ya kawaida ya uzazi wa panya hao.
Uchunguzi huu unamaanisha kuwa siku za usoni huenda wanawake wasishirikishwe katika utengenezaji wa watoto kabisa, watafiti wanasema kwenye matokeo ya utafiti huo ambayo yamechapishwa kwenye jarida la kimatibabu la Nature Communications.
Wanasayansi hao kutoka Chuo Kikuu cha Bath walianza majaribio hayo kwa kutumia mayai ya uzazi ambayo hayajatungishwa mbegu za kiume.
Walitumia kemikali kufanya ujanja fulani ambao ulielekeza mayai hayo ya uzazi kuwa makamilifu.
Mayai haya ya bandia yanafanana au yana sifa nyingi zilizo sawa sana seli za kawaida kama vile seli za ngozi, katika njia ambayo zinajigawanya na pia kudhibiti chembe zinazoamua maumbile ya viumbe au DNA.
Watafiti wanasema kuwa iwapo kwa kutungisha mbegu za kiume kwenye mayai bandia kunaweza kuzalisha watoto wenye afya kwa panya, basi inamaanisha kuwa siku za usoni mpango huo unaweza ukatumiwa kwa mwanadamu na kwa kutumia seli ambazo ambazo hazitoki kwenye mayai ya uzazi.
Katika majaribio ya panya, uwezekano wa upachikaji mimba uliweza kufaulu mara moja kwa kila mara nne. Hii ni sawa na asilimia 25.
Dkt Tony Perry, mmoja wa watafiti hao aliambia BBC kuwa: "Hi ni mara ya kwanza kwa mtu yeyote kuweza kuthibitisha kwamba kitu kingine chochote, isipokuwa mayai ya uzazi, kinaweza kuungana na mbegu za kiume ili kuzalisha mtoto. Hali hii inafutilia mbali dhana ambayo imekuwepo kwa zaidi ya miaka 200."
Panya waliozaliwa kwa njia hiyo walikuwa na afya, walikuwa na maisha marefu kama panya wengine wa kawaida na waliweza kuzaa baadaye watoto wa kawaida.
Iwapo haja ya kuwa na yai ili kuzalisha itaondolewa kutakuwepo na mabadiliko mengi katika jamii.
Wanaume wawili kuzaa
Dkt Perry alisema: "Kuna uwezekano mkubwa kuwa siku za usoni seli za kawaida mwilini zitachanganywa na mbegu za kiume ili kuunda yai lililotungishwa mbegu."
Hii inamaanisha kuwa, wanaume wawili wanaweza kuzaa mtoto, ambapo mmoja wao atatoa seli na mwingine achangie mbegu za kiume.
Katika hali nyingine mwanamume anaweza kumzaa mtoto wake yeye mwenyewe kwa kuwa ataweza kutumia seli zake na mbegu zake yake kwa shughuli hiyo muhimu.
Hapa mtoto anayezaliwa atakuwa kama pacha wa babake badala ya kuwa kiumbe kinachofanana naye.
Hata hivyo Dkt Perry anasema kuwa dhana hizi, kwa wakati huu, ni za matumaini tu.
Mapema mwaka huu nchini Uchina, wanasayansi waliweza kutengeneza mbgeu za kiume kutoka seli tete na kisha kutumia mbegu hizo kuzalisha panya wenye afya.
Dkt Perry alipendekeza kuwa utafiti huo unavyoendelea sambamba, unaweza ukafikia mahali ambapo mayai ya mama na mbegu za wanaume visihitajike kabisa katika uzalishaji au utengenezaji wa watoto.

MJUE MZEE MWENYE UMRI WA MIAKA 145

13:25 Add Comment

Mzee huyu kwa jina Mbah Ghoto kutoka Indonesia anaamini ndiye binadamu mzee zaidi kuwahi kuishi duniani.
Anasema ameishi muda zaidi kushinda wake zake wanne, ndugu zake 10 na wanawe wote.
Anatokea kisiwa cha Java ya Kati.
"Huwa najaribu kuwa mvumilivu na kuamini kuwa kuna watu watakaonitunza," ameambia BBC.
"Nimeishi muda mrefu kwa sababu nina watu wanaonipenda na kunitunza."
Yeye bado huvuta sigara.
Mjukuu wake Suryanto anasema kwa mujibu wa stakabadhi rasmi za serikali, Mbah Gotho ana miaka 145. Alizaliwa 31 Desemba 1870.
"Tunaamini stakabadhi hizi ni halali, kwa mujibu wa nyaraka rasmi za serikali. Tunaamini tarehe yake ya kuzaliwa ni sahihi," anasema afisa wa serikali Wahyu Wiyanto.
Indonesia ilianza kunakili rasmi kuzaliwa kwa watu 1900 hivyo ni vigumu kuthibitisha tarehe kamili ya watu waliozaliwa kabla ya hapo.
Na kumewahi kutokea makosa awali.
Lakini Mbah Gotho anachukuliwa kama shujaa eneo analotoka.
"Siku ya Uhuru alikuwa akialikwa kusimulia yaliyotokea wakati wa vita. Anaweza kusimulia kuhusu vita dhidi ya wakoloni kutoka Japan na Uholanzi," anasema Wahyu Wiyanto.
Mjukuu wake anasema mzee huyo huwa hana masharti mengi na huwa haitishi chakula maalum.
"Kitu pekee alitutaka tufanye ni kununua jiwe la kaburi lake," anasema.
Mzee huyo anasema kwa sasa anaishiwa na nguvu na hawezi kutarajia aishi muda mrefu zaidi.
"Sina nguvu kama zamani. Hata kutembea ni shida. Nilikuwa mkulima na nilivua samaki mtoni. Sitaki kuendelea kuishi sana, ndio maana nimeandaa kaburi. "Ili nikifariki, kila kitu kiwe tayari," anasema.
"Kwa sasa nataka tu kufariki, lakini wakati wangu haujafika bado."
Mtu ambaye aliishi miaka mingi zaidi duniani kulingana na Guinness ni Jeanne Calment kutoka ufaransa ambaye aliishi miaka 122 na siku 164 . Aliaga dunia mwezi Agosti mwaka 1997.

WAZIRI MKUU DRC AJIUZULU

06:34 Add Comment

Waziri mkuu nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Augustin Matata Ponyo, amejiuzulu na kutoa fursa ya kuteuliwa mrithi wake kuongoza serikali ya mpito.
Kujiuzulu kwa bwana Ponyo ni sehemu ya makubaliano yaliyotiwa sahihi mwezi uliopita kati ya serikali ya Rais Joseph Kabila na baadhi ya vyama vya upinzani ya kuhairisha uchaguzi wa urais hadi mwezi Aprili mwaka 2018.
Wapiga kura nchini DRC walistahii kupiga kura mwezi huu kumchagua mrithi wa Rais Kabila, wakati wa kumalizika kwa muhula wake wa mwisho.
Vyama vikuu vya upinzani vinakataa kuhairishwa kwa uchaguzi vikisema kuwa hiyo ni njama ya Rais Kabila ya kusalia madarakani.
Baraza lote la mawaziri lilijiuzulu pamoja na bwana Ponyo.

MWEZI MKUBWA ZAIDI UNATARAJIWA KUONEKANA DUNIANI

12:47 Add Comment

Watazamaji wa anga wanajiandaa kuuona mwezi mkubwa zaidi wakati ambapo utakaribia dunia tangu 1948.
Uingereza itakuwa na fursa nzuri kuuona mwezi huo siku ya Jumatatu jioni,licha ya kuwa utakaribia dunia mwendo wa saa tano na dakika 21 muda wa GMT ambapo utakuwa umbali wa kilomita 356,509.
Wachunguzi watauona mwezi huo kuwa mkubwa zaidi kwa asilimia 7 ukilinganishwa na mwezi wa kawaida na kung'aa zaidi ya asilimia 15, licha ya kwamba macho ya binaadamu yanaweza kupambanua tofauti hiyo.
Huku mwezi huo ukitarajiwa kutokaribia dunia hadi tarehe 25 mwezi Novemva 2034, idara ya maswala ya hewa nchini Uingereza imesema kuwa kutakuwa na mawingu mazito wakati mwezi huo utakapokaribia.
Huku mwezi ukizunguka dunia,kuna tofauti ya mwangaza unaotolewa na jua.Ni wakati huo ambapo mwezi wote humulikwa na mwangaza huo na kutoa mwezi mkubwa zaidi.

TRUMP AFANYA UTEUZI WA AWALI

05:57 Add Comment

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amemteua mwenyekiti wa kamati ya taifa ya chama cha Republican, Reince Priebus, kutumika kama mkuu wa wafanyakazi.
Bwana Priebus ana uhusiano wa karibu na spika wa baraza la wawakilishi Paul Ryan. Wandishi wa wa habari wanaarifu kwamba uteuzi wa Piebus unaweza kuwaudhi wafuasi wake wa hali ya chini na hii inaashiria kwamba uongozi ujao unalenga kufanya kazi kwa karibu na baraza la Congress kujihakikishia ushindi wa mapema wa baraza hilo.
Stephen Bannon, alikuwa ni mwenyekiti wa taasisi ya Breitbart News, ambayo ni tovuti yenye maoni ya mrengo wa kulia , naye ameteuliwa kwa nafasi ya mkuu wa mipango na mshauri mwandamizi.
Mkuu wa wafanyakazi ambaye anafanya kazi kama mruhusu na mtengeneza ajenda kwa rais, na kwamba ni mmoja wa chaguo muhimu la mapema kwa rais ajae.
Katika taarifa yake, Trump alinukuliwa akiwazungumiza Priebus na Bannon ni viongozi wenye sifa za hali ya juu waliofanya kazi pamoja wakati wa kampeni zake za kuingia Ikulu ya Marekani.

TRUMP KUWAREJESHA WAHAMIAJI KWAO

05:55 Add Comment

Donald Trump asema kati ya wahamiaji haramu milioni mbili ama tatu watasafirishwa kutoka Marekani baada ya kuapishwa kuwa rais wa chi hiyo.
Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Marekani,CBS, Trump amesema wahamiaji wote wenye rikodi za uhalifu, ikiwemo makundi ya wahalifu na walanguzi wa dawa za kulevya ndio watakuwa kipaumbele chake .
Hatma ya wahamiai haramu milioni nane na ushee waliosalia itafahamika mara tu mpaka utakapokuwa salama.
Donald Trump ameongeza kuwa semhemu ya ukuta ambao aliahidi kujenga kwenye mpaka baina ya nchi yake na Mexico, unaweza kuwa ni uzio.

TRUMP AWASILI WHITE HOUSE

20:15 Add Comment

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amewasili katika Ikulu ya White House, kwa mujibu wa maafisa nchini Marekani.
Hata hivyo aliingia akitumia mlango tofauti na kuwasili kwake hakukunaswana kamera za waandishi wa habari.
Anatarajiwa kuwa kwenye mazungumzo na Rais Obama wakati huu.
Licha ya tofauti zao, bwana Obama siku ya Jumatano alikishauri kikosi chake kufanya jitihada zaidi kuhakisha kuwa kuna mafanikio kwenye shughuli ya kupokeza madaraka kwa Republican mwezi Januari.
Mapema kikosi cha kampeni ya Trump kilikutana na washauri kujadili masuala kuhusu siku za kwanza 100 za Trump kama rais na uteuzi muhimu katika nyadhifa za serikali.
Majina yaliyotajwa ni kati ya wale waliomuunga mkono Trump kutoka mwanzo akiwemo aliyekuwa spika Newt Gingrich, maseneta Jeff Sessions na Bob Corker pamoja na aliyekuwa meya wa New York Rudy Giuliani.

TRUMP AONGOZA KWA KURA

06:34 Add Comment
Mgombea wa Urais wa Marekani wa chama cha Republican, Donald Trump akizungumza kwenye mdahalo wa tatu uliofanyika Jumatano
Katika mdahalo wa tatu na wa mwisho uliofanyika Jumatano hii, mgombea huyo kupitia chama cha Republican, amesema ana wasiwasi kura zitaibiwa. Amedai kuwa mpinzani wake, Hillary Clinton wa chama cha Democratic, hakutakiwa hata kuwania nafasi hiyo.