FOOTBALL FREESTYLES KUANZA KUTIMUA VUMBI MWEZI HUU

06:23

Dar es Salaam. Mashindano ya Taifa ya mchezo wa kuonyesha ufundi wa kuchezea mpira wa miguu nchini yanatarajiwa kuanza rasmi Novemba 19 kwenye Viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam.
Lengo la mashindano hayo yanayofanyika kwa mara ya kwanza nchini ni kutafuta bingwa atakayeiwakilisha nchi kwenye mashindano ya dunia mwakani.
Mratibu wa mashindano hayo, Jacob Mbuya alisema wanaoruhusiwa kushiriki ni wale wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.
“Mashindano yatafanyika kwa nchi nzima, lakini kwa kuanzia, tutazihusisha wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni hapa Dar es Salaam ili tuone mwitikio wa watu ukoje,” alisema Mbuya.
Katibu wa chama hicho Tanzania (FFT), Morison Mosses alisema kuwa fomu za kushiriki mashindano hayo tayari zimeshaanza kutolewa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »