UCHAMBUZI MECHI YA SIMBA DHIDI YA KAGERA SUGAR

20:03

Simba inarudi nyumbani Dar es Salaam, ikiwa salama baada ya ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Mbeya City katika pambano lililopigwa Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya
Kocha Joseph Omog, Jumamosi atakuwa katika nafasi nzuri ya kujitanua kileleni mwa msimamo wa ligi ya Vodacom, Tanzania wakati watakapo wakaribisha Kagera Sugar ya Bukoba kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Simba inarudi nyumbani Dar es Salaam, ikiwa salama baada ya ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Mbeya City katika pambano lililopigwa Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kinyume na matarajio ya Simba kwani Kagera Sugar siyo timu ya kubeza kwani imekuwa ikiisumbua mara kwa mara Simba bila kujali ni uwanja gani wanapocheza na mbaya zaidi timu hiyo msimu huu inafundishwa na kocha Mecky Maxime, kocha mwenye uwezo mkubwa wa kuusoma mchezo.
Kagera nao wanaingia kwenye mchezo huo wakijivunia ushindi wa ugenini wa bao 1-0, dhidi ya vibonde Majimaji matokeo ambayo yaliwapandisha hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa na pointi 15 nne nyuma ya Simba.
Simba wataingia kwa nguvu katika mchezo wa kesho kuhakikisha wanapata ushindi utakaozidi kuwaweka kwenye nafasi nzuri ya kuongoza ligi hiyo na kuwaacha mbali wapinzani wake Stand United na mabingwa watetezi Yanga ambao wanatofautiana kwa pointi sita na mchezo mmoja.
Kocha Omog huenda akamkosa mfungaji wake Shizza Kichya aliyeumia kifundo cha mguu katika mchezo uliopita na kulazimika kutolewa nje dakika ya 81, na taarifa za daktari wa timu hiyo Yassin Gembe amesema bado anaendelea kufatilia kwa karibu afya ya mchezaji huyo kama ataweza kurudi uwanjani.
Mshambuliaji Laudit Mavugo anatarajia kurudi kwenye kikosi cha kwanza baada ya kuanzia benchi katika mchezo uliopita na niwazi kitendo cha kuanzishwa benchi kitakuwa kimemkera hasa baada ya timu kucheza vizuri na kupata ushindi hivyo atacheza kwa juhudi kutaka kufunga ili kurudisha imani kwa kocha.
Safu ya ulinzi inatarajiwa kubaki kama ilivyokuwa katika michezo miwili iliyopita ambapo Maimbabwe Method Mwanjali na Novaty Lufunga wakianza huku Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude na Mzamiru Yasini wakianza kwenye eneo la kiungo wakifanya kazi yao nzuri katika kuwalisha mipira washambuliaji wa timu hiyo.
Ibrahim Ajibu mfungaji wa bao la kwanza kwenye mchezo na Mbeya City anatarajiwa kuendeleza makali yake kwa kuwasumbua mabeki wa timu pinzani na kutengeneza nafasi kwa Mavugo au Blagnon ambao ndiyo wanaotegemewa katika umaliziaji.
Mfumo ambao unatarajiwa kutumiwa na kocha Omog , ni ule wa 4-4-2, ambao kocha huyo ametamba kuwa ndiyo mfumo sahihi unaompa matokeo hasa wanapocheza nyumbani.
Kwaupande wake Meneja wa Kagera Sugar Mohamed Husseni amesema wamekuja Dar es Salaam kwa lengo moja tu nalo ni kupata pointi tatu na hiyo ni baada ya kuwafahamu vizuri wapinzani wao Simba.
Husseni, amesema wanataka kuwa timu ya kwanza kuisimamisha Simba tena kwenye uwanja wa nyumbani na hilo linawezekana kwakua wachezaji waliokuwa nao hawana tofauti na wale wa wapinzani wao Simba.
“Tunajulikana kwa upinzani tunapocheza na Simba, iwe hapa Dar es Salaam au Kaitaba kule Bukoba, tumekuwa tukiwasumbua na kupata matokeo ingawa msimu uliopita walitufunga mechi zote mbili lakini msimu huu tumejipanga kuhakikisha tunakumbushia kile tulichokifanya misimu miwili iliyopita tuliwafunga na watu walingoa viti uwanjani,”amesema Husseni.
Kiongozi huyo amesema kikosi chao kipo tayari kwa mchezo huo na hawana mchezaji yeyote aliyekuwa majeruhi na anauhakika watacheza kwa kujituma kwa kutumia mbinu za kocha Maxime ili kupata ushindi ambao kwao ni muhimu kutokana na kasi waliyoanza nayo msimu huu.
“Tunajenga timu chini ya kocha Maxime, lakini tunafurahi na mwenendo wetu tulioanza nao naamini hata keshi mambo yatakuwa mazuri tutapata matokeo hapa Dar es Salaam kwani tunarekodi ya kuzisumbua timu hizi mbili kubwa,’amesema Husseni.
Kocha Maxime amekuwa akitumia mfumo wa 4-5-1 hasa anapocheza ugenini na anaamini utampa matokeo mazuri katika mchezo huo kwa kujaza viungo wengi ili kuwadhibiti Simba ambao wanatengeneza mashambulizi yao kupitia katikati ya uwanja.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »