MTOTO WA ZLATAN AJIUNGA NA AKADEMI YA MANCHESTER UNITED

19:56

Imeripotiwa kuwa vijana wawili wa mshambulizi wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic wamejiunga na akademi ya klabu anayoichezea baba yao
Kwa mujibu wa The Sun, kijana wa miaka kumi wa raia huyo wa Sweden Max na kijana wake mwingine wa miaka nane Vincent wameanza mazoezi na kocha wa United wa vijana wadogo wiki za hivi karibuni pamoja na mtoto wa Wayne Rooney wa miaka sita Kai.
"Tumaini la klabu ni kwamba baadhi ya vipaji vya baba yao vinaweza kuwemo kwa vijana hao," chanzo kililiambia gazeti.
"Manchester United wanafahamika kwa ubora wao katika kukuza vipaji, na hii ni hatua nyingine katika harakati za kutafuta mastaa wa baadaye. United ina makocha bora wa watoto duniani, na wachezaji wanajua kwamba wapo mahali sahihi."
Michael Carrick, Ryan Giggs na Nicky Butt wamesajili watoto wao kwenye akademi ya United.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »