Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amepokelewa kwa heshima za kijeshi nchini Ethiopia. Katika mji mkuu Addis Ababa, amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu Hailemariam Desalegn. Merkel ametaka watu waruhusiwe kuandamana na polisi watumie mbinu sahihi kuwadhibiti. Jumapili iliyopita, serikali ya Ethiopia ilitangaza hali ya hatari baada ya machafuko kuzuka. Waziri Mkuu Desalegn amekanusha shutuma kuwa vyombo vya usalama vilitumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji. Akiwa Addis Ababa, Merkel amepanga pia kukutana na wawakilishi wa upinzani na kuzindua jengo jipya la makao makuu ya Umoja wa Afrika. Ujerumani ilichangia Euro milioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Ethiopia imetoa hifadhi kwa wakimbizi zaidi ya 740,000 kutoka Sudan Kusini, Somalia na Eritrea na hivyo kuifanya kuwa moja ya nchi kumi zenye wakimbizi wengi zaidi duniani.
EmoticonEmoticon