IDADI YA WASICHANA WANAOOLEWA KATIKA UMRI MDOGO YAONGEZEKA

18:02

Shirika la kimataifa la kutetea haki za watoto, Save the Children, limeonya kuwa idadi ya wasichana wanaoolewa wakiwa na umri mdogo inaongezeka. Hayo ni matokeo ya ripoti ya shirika hilo iliyozinduliwa leo, ikiwa ni Siku ya Mtoto wa Kike Duniani. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, wapo wanawake na wasichana milioni 700 duniani, wanaoishi katika ndoa zilizofungwa walipokuwa bado hawajafikisha miaka 18. Shirika la Save the Children linakadiria kuwa hadi kufikia mwaka 2050, idadi hiyo inaweza kupanda na kufikia bilioni 1.2. India inaongoza kwa ndoa za watoto. Nchini humo, asilimia 47 ya wasichana huolewa wakiwa na umri chini ya miaka 18. Katika nchi hiyo, sawa na Afghanistan, Yemen na Somalia, baadhi ya wasichana wanaolewa hata kabla hawajafikisha miaka 10.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »