MAHAKAMA ya Mkoa Chake chake, imeanza kusikiliza utetezi wa mshitakiwa Seif Abeid Mohamed (22) Mkaazi wa Jondeni Mkoani Pemba, alieshitakiwa kwa kosa la kubaka msichana wa miaka (12), ambapo alidai mbele ya mahakama kutohusiki na kesi hiyo bali linaloendele ni kutokana na chuki kwa baba wa mlalamikaji na ameweza kumpa kosa lisilomuhusu.
Alidai kuwa, hana mazoea na mlalamikaji na kumfahamu kwake ni kumuona njiani tu katika maisha yake anayoishi isipokuwa baba wa mlalamikaji anahasira nae ndio alipoamua kumpa kesi hiyo ili kumtia mashakani.
Alidai , siku ya tukio hilo alikua akitoka Bandarini Kastam akienda Jondeni njiani alimkuta baba wa mlalamikaji na kumwambia kuwa anamchukulia mwanawe mshitakiwa huyo baada ya kumkatalia baba wa mlalamikaji alidai kuwa atamshitaki.
Mshitakiwa baada ya kukamilisha utetezi wake mwendesha mashitaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa mashitaka Pemba (DPP) Seif Mohamed Khamis, alimuuliza mshitakiwa, mlalamikaji anamfahamu mshitakiwa alidai kuwa anamfahamu kwa kumuona tu na masafa anayoishi mshitakiwa na anapoishi mlalamikaji ni mbali.
Hakimu wa makahama hiyo, Khamis Ali Simai, alifunga ushahidi wa mshitakiwa huyo kutokana na mshitakiwa kudai kuwa hana shahidi wa kumleta mahakamani, shauri hilo limeahirishwa tena hadi Novemba 9 mwaka huu mshitakiwa atakaporudi tena mahakamani hapo kwa ajili ya hukumu.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo mshitakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 3 mwaka 2014 majira ya saa 1:30 usiku, Jaalani Mkoani Pemba, kwa makusudi bila ya halali na bila ya ridhaa alimbaka msichana mwenye umri wa miaka 12 na kumsababishia maumivu katika sehemu zake za siri.
Ambapo kutenda kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 125 (1) (2) (e) na 126 (1) cha Sheria namba 6 ya mwaka 2004 sheria ya Serikali ya Zanzibar.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon