Dar es Salaam. Kutotimia kwa akidi ya wakunga katika hospitali na vituo vya afya nchini ni chanzo mojawapo cha vifo vya wajawazito.
Hayo yamesemwa wakati wa matembezi ya hisani ya kuchangisha fedha kwa ajili ya mafunzo ya wauguzi na wakunga yaliyoandaliwa na Shirika la Amref Afrika kwa kushirikiana na Benki M (Tanzania).
Akizungumza baada ya matembezi hayo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema lengo la Serikali ni kupunguza vifo hivyo kwa zaidi ya nusu na baadaye kuvimaliza kabisa.
“Idadi ya madaktari ni kubwa na inatosha. Tatizo lililopo sasa ni idadi ndogo ya wakunga. Tukiweza kupata wataalamu hao, nchi itapiga hatua kwa kupunguza vifo vya kinamama hadi kufika 200 kwa mwaka,” amesema.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa mgeni rasmi katika matembezi hayo, amesema vifo hivyo vimepungua kutoka 432 kwa mwaka hadi 410, idadi ambayo alisema bado ni kubwa.
“Sisi Wanawake tunaokwenda ‘labor room’ kwa ajili ya kufanya kazi tuliyotumwa na Mungu ya kuleta uhai duniani, hatupaswi kufa kwa sababu ambazo zinaweza kuepukika,” amesema Suluhu.
Alisema Serikali ilishindwa kutimiza malengo ya milenia kwa mwaka 2015 ya kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa asilimia 75 kama ilivyoahidi, lakini imejiwekea mikakati madhubuti ili kutimiza Malengo Endelevu ya Sasa (SDGs 2030).
Taarifa hiyo imekuja wakati takwimu zikionyesha wanawake 23 na watoto 144 hufariki dunia kila siku nchini, huku watoto wachanga 410 wakipoteza maisha kati ya vizazi hai 100,000.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon