YANGA inaweza kunyimwa leseni ya kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani kama haitatimiza masharti yalipo kwenye leseni hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema mwisho wa kujaza fomu za kushiriki mashindano hayo ni Novemba 30 mwaka huu.
“TFF tunatarajia kutuma Yanga kama mshiriki wa Ligi ya Mabingwa na Azam FC kama mshiriki wa Kombe la Shirikisho na ili timu ipate leseni lazima iwe imetimiza masharti ya leseni za klabu,” alisema Lucas.
Pia lisema CAF wapo makini kwani wanafuatilia kwa karibu kuona kile ulichokieleza kama unacho ili kukwepa kupanga matokeo.
Lucas alisema upangaji wa matokeo hauko upande mmoja tu hata kutokuwa na miundombinu mizuri ya kufanya mazoezi na mambo ya utawala kunaweza kuiathiri timu isifanye vizuri.
Kwa mujibu wa masharti ya leseni za klabu mmiliki mmoja anatakiwa kumiliki klabu mmoja, kuwa timu inatakiwa kuwa na uwanja wa mazoezi, na watendaji wake.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon