MATOKEO YA MECHI ZA LEO LIGI KUU YA UINGEREZA

20:20

Mabingwa watetezi wa Lig ya Premia Leicester City wamecharazwa 3-0 na Chelsea uwanjani Stamford Bridge nao Arsenal wakafanikiwa kuondoka na ushindi dhidi ya Swansea City licha ya kusalia na wachezaji 10 uwanjani.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Diego Costa, Eden Hazard na Victor Moses.
Theo Walcott alifunga mawili upande wa Arsenal kabla ya Gylfi Sigurdsson kukomboa moja upande wa Swansea.
Mesut Ozil aliwarejesha Arsenal mabao mawili mbele baada ya kufikia krosi ya kabla ya nguvu mpya Borja Baston kufunga la pili upande wa Swansea.
Granit Xhaka wa Arsenal alioneshwa kadi nyekundu lakini wakafanikiwa kukwamilia ushindi wao.
Uwanjani Etihad, vijana wa Pep Guardiola wametoka sare 1-1 na Everton. Everton walitangulia kufunga kupitia Romelu Lukaku. City walikomboa kupitia Nolito.
Mechi iliyoshangaza wengi ni ya Bournemouth ambao wamepata ushindi mkubwa wa 6-1 dhidi ya Hull City.
Matokeo kamili ya mechi za leo
Arsenal 3-2 Swansea
Bournemouth 6-1 Hull
Man City 1-1 Everton
Stoke 2-0 Sunderland
West Brom 1-1 Tottenham
Chelsea 3-0 Leicester city

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »