NGASA ACHAMBUA UDHAIFU WA YANGA

06:59

KIUNGO mshambuliaji wa zamani wa Yanga anayechezea Mbeya City, Mrisho Ngassa amesema Yanga inahitaji wachezaji wawili wa kuchezesha timu ili kuwa na uwiano mzuri.
Akizungumza na gazeti hili, Ngassa alisema Yanga inahitaji wachezaji wenye uwezo wa kuuchezea mpira na kutoa pasi za mwisho.
“Ukiangalia Yanga wanavyocheza kwa sasa, unaona kabisa inakosa watu wa kuchezea mpira na kutoa pasi za mwisho kama alivyo Haruna Niyonzima ili wawe na uwiano mzuri katika timu, lazima wawapate hao watu,”alisema Ngassa.
Pia Ngassa alisema sababu hiyo ndio chanzo cha Yanga kufanya vibaya katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Simba.
“Mechi ilikuwa nzuri, Simba waliwazidi Yanga katikati kwani walikuwa wanacheza mipira mirefu kumtumia Msuva peke yake, hivyo Simba wakagundua njia hiyo, baada ya kusogea pembeni wakaua mipango ya Yanga,” alisema Ngassa.
Ngassa alisema wachezaji wengi wa Yanga kwa sasa wamechoka baada ya kucheza michezo mingi ya kimashindano, hivyo miili yao inahitaji kupumzika.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »