Uongozi wa Klabu ya Azam FC umethibitisha kuachana na beki wake raia wa Ivory Coast, Serge Wawa ambaye leo amejiunga na timu ya El Merreikh ya Sudan kwa mkataba wa miaka miwili.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Iddi alisema Wawa anaondoka Azam kama mchezaji huru baada ya mkataba wake wa miaka miwili na klabu hiyo kumalizika.
"Mkataba wa Wawa na Azam FC umemalizika na uongozi haukuona haja ya kumpatia mpya. Sisi Azam tunamtakia kila la kheri na tupo katika mchakato wa kuituma haraka hati yake ya uhamisho ya kimataifa (ITC) ili aanze kuitumikia klabu yake mpya," alisema Iddi.
Wakati huohuo, Iddi alisema klabu hiyo imetoa mapumziko ya wiki mbili kwa wachezaji wake baada ya kumaliza mechi mbili za kirafiki dhidi ya timu za JKT Ruvu na Ruvu Shooting.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon