AJIB KUSEPA MSIMBAZI

07:45

Wakati mkataba wake wa kuitumikia Simba ukielekea ukingoni, mshambuliaji Ibrahim Ajib amebainisha kuwa mwelekeo wake wa kisoka ni baada ya kumalizana na klabu hiyo mwakani.
Ajib ambaye amekuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kocha Joseph Omog aliliambia gazeti hili jana kwamba hajafikiria kuongeza mkataba na timu hiyo au kwenda kwingine.
“Mkataba wangu utakwisha mwakani na kanuni zinaniruhusu kufanya mazungumzo na timu nyingine kwa kipindi hiki, lakini natakiwa nitulie na kutafakari kwa upana suala hili.
“Upande wa Simba SC, bado sijafikiria kuongeza mkataba, nahitaji kwanza niutumikie huu niliona, umalizike ndipo nitajua nini cha kufanya, binafsi soka ndiyo kila kitu kwangu, hivyo mkataba niliona utakapokwisha nitakuwa ninajua mwelekeo wangu uko vipi,” alisema Ajib.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »