YANGA YASHUSHA PUMZI

05:32

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu bara, Yanga, jana walishusha pumzi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Toto Africans ya mjini hapa.
Ushindi huo unaifanya Yanga kupanda mpaka nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 18 sawa na Kagera Sugar iliyo nafasi ya nne.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, timu hizo zilikuwa zikishambuliana kwa zamu katika vipindi vyote viwili.
Mshambuliaji Obrey Chirwa aliendelea kupata mabao kwa timu yake hiyo, baada ya kufunga bao la kuongoza katika dakika ya 28.
Chirwa alikuwa kwenye shinikizo kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo waliokuwa wakimlalamikia kushindwa kufunga, lakini aliondoa jinamizi hilo k w e n y e mechi yao dhidi ya Mtibwa S u g a r a m bapo a l i fung a b a o katika ushindi wa mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
C h i r w a alifunga bao hilo la kichwa baada ya kuun ganisha pasi ya Simon Msuva. Dakika ya 55, Msuva aliifungia Yanga bao la pili kwa mkwaju wa penalti.
Mwamuzi Andrew Shamba wa Pwani alitoa penalti hiyo baada ya Deus Kaseke kuangushwa eneo la hatari na Ramadhan Malima wa Toto.
Kutoka kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, Majimaji ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji African Lyon.
Wafungaji wa Majimaji kwenye mechi hiyo walikuwa Peter Mapunda dakika ya 64 na Marcel Bonaventure katika dakika ya 73. Kwa ushindi huo, Majimaji imesogea kwa nafasi moja na sasa iko nafasi ya 15 ikiwa na pointi tisa. Toto imeshuka mkiani ikiwa na pointi 8.
Katika mechi iliyochezwa uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara, Ndanda ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya City huku Prisons ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Stand United kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.
Prisons sasa imechupa mpaka nafasi ya sita ikiwa na pointi 15 na Stand imebaki nafasi yake ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi zake 20. Nayo Ruvu Shooting ikiwa nyumbani kwenye uwanja Mabatini, ilitoka sare ya bao 1-1 na Mwadui.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »