Klabu ya Yanga Sc leo imetangaza kuahirisha mkutano wake mkuu uliopangwa kufanyika kesho jijini Dar es Salaam baada ya baadhi ya wanachama wake kwenda mahakamani kupinga mkutano huo kufanyika.
Mwenyekiti wa Yanga Sc, Yusuph Manji amewaambia waandishi wa habari kuwa, jana alipokea barua ya pingamizi la mkutano huo kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,na kwamba ameamua kutii agizo hilo la mahakama hadi itakapofanya maamuzi yake.
Manji amewataka wanachama wa mikoani ambao walipanga kuja Dar es Salaam kuhudhuria mkutano huo, kusitisha safari yao hadi itakapopangwa tarehe nyingine.
Hata hivyo, Manji amedai kuwa waliokwenda mahakamani kupinga kufanyika kwa mkutano huo uliolenga kufanya makabidhiano ya timu hiyo kwa kampuni ya Yanga Yetu ambayo Mkurugenzi wake ni Manji, si wanachama halali kwa kuwa walifutwa uanachama wao.
“Naomba wanayanga mtusamehe tumelazimika kuhairisha mkutano wa kesho baada ya kupokea oda ya mahakama, tunaishi kwa kufuata sheria za nchi hatuna budi kutii agizo la mahakama. Ila tutapeleka vithibitisho vyetu mahakamani ili kulipatia ufumbuzi pingamizi hilo, mmeniamini na kunichagua kwa demokrasia msijali haya yatakwisha na wanayanga mtapata fursa ya kuamua hatima ya kimaendeleo kwa masilahi ya klabu yetu,” amesema Manji.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon