KAMATI YA BUNGE YAKATAA RIPOTI YA WIZARA

05:34

Dodoma. Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imekataa kupokea ripoti ya umwagaji wa taka zenye sumu baada ya wajumbe wake kushindwa kutembelea miradi kwa kile kinachodaiwa ni ukosefu wa fedha.
Mbunge wa Konde (CUF), Khatib Said Haji aliomba suala hilo lisijadiliwe kwa sababu wabunge hawajaenda katika maeneo hayo kujionea uhalisia na kuzungumza na upande mwingine ambao ni wananchi.
“Hakuna tunalolijua. Tushauri jambo ambalo hatulijui? Ukishauri kitu usichokijua utakuwa mshauri hewa na hii ina athari kubwa,” alisema.
Ripoti hiyo ilikuwa iwasilishwe jana na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina katika kamati hiyo na kisha kujadiliwa na wajumbe.
Hata hivyo, kabla ya kuwasilishwa, makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Vicky Kamata aliruhusu wajumbe kuzungumzia kuhusiana na ripoti hiyo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »