BOMOABOMOA ya nyumba na majengo ya wananchi katika eneo la Maili Moja waliojenga kwenye hifadhi kuanzia katikati ya Barabara ya Morogoro kwenye eneo la Kiluvya hadi Tamco, Maili Moja wilayani hapa sasa inatarajiwa kufanyika Januari 23, mwakani.
Ubomoaji huo ambao awali ulipangwa kufanyika mwezi ujao na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Pwani ulikuwa unagusa soko la Maili Moja la mkoa ambalo nalo liko kwenye hifadhi ya barabara.
Akizungumza na wananchi na wafanyabiashara waliojenga katika hifadhi hiyo ya barabara, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo alisema wafanyabiashara hao hawataondolewa hadi Halmashauri ya Mji wa Kibaha itakapowajengea soko lingine.
“Tayari maelekezo yametolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwamba bomoabomoa ni mita 60 na siyo 120 kama ilivyoonyesha na kutangazwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Pwani,” alisema Ndikilo.
Alisema ujenzi wa soko utafanyika eneo la Mnarani maarufu kama Sagulasagula au Loliondo ambako kutakuwa na huduma zote ikiwemo ya maji.
Alibainisha kuwa muda uliopangwa wa miezi mitatu sawa na siku 90 vitu vyote viwe vimekamilika na kwamba hautaongezwa tena, hivyo waliojenga eneo la hifadhi ya barabara waanze kuvunja wenyewe kabla ya muda uliopangwa haujafika.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani Pwani, Abdallah Ndauka alishukuru msimamo wa Mkuu wa Mkoa wa kutoa muda wa nyongeza ili waweze kutekeleza agizo hilo la halmashauri.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon