AZAM FC YATAJA SABABU ZA KUANZA MSIMU VIBAYA

12:48

Azam waanika sababu za kuaanza msimu vibaya na kocha ni hausiki
Uongozi wa klabu ya Azam FC, umesema licha ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu yao kwenye ligi ya Vodacom, lakini wataendelea kuwapa nafasi makocha wao kutoka Hisapnia kuifundisha timu hiyo.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ameiambia Azam waanika sababu za kuaanza msimu vibaya, mwenendo huo ni wakwanza kuikumba klabu yao kwa misimu nane tangu walipoanza kushiriki kwa mara ya kwanza ligi hiyo lakini hawana budi kuwapa muda makocha hao kwakua bado hawajaizoea ligi.
“Ni kweli tumeanza vibaya msimu huu lakini tatizo siyo makocha wapya tatizo ni majeruhi tuliokuwa nao lakini pia makocha bado wanaendelea kufanya mabadiliko ya taratibu ndani ya timu kwahiyo lazima tuwape muda hadi kumalizika kwa mzunguko wa kwanza ili kuona kama kutakuwa na mabadiliko,”amesema Kawemba.
Kiongozi huyo amesema lengo la kufanya hivyo ni kuepuka kuwachanganya wachezaji endapo wataleta kocha mpya na ndiyo maana wakafikia maamuzi hayo ya kuwapa muda Wahispania hao ambao wameshinda mechi tatu tangu kutua msimu huu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »